TAARIFA hii inahitimisha mfululizo wa taarifa za
kilichokuwa Kimbunga “IALY” zilizokuwa zikitolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA) tangu tarehe 17 Mei 2024. Mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa
unaonesha kuwa katika kipindi cha saa 6 zilizopita, Kimbunga “IALY” kimepoteza kabisa
nguvu yake, kikiwa kaskazini mashariki mwa pwani ya Kenya.
Hivyo, kwa sasa hakuna tena tishio la kimbunga “IALY”
katika nchi yetu. Aidha, wakati kikipita karibu na pwani na nchi yetu kati ya
jana tarehe 21 na leo tarehe 22 Mei 2024 kimeweza kusababisha vipindi vya mvua,
upepo mkali na mawimbi makubwa katika maeneo ya pwani ya nchi yetu kama
ilivyotabiriwa awali.
Hata hivyo ikumbukwe kuwa, japo tunaelekea mwishoni
mwa msimu wa Masika, 2024, tunakaribia kuanza kwa msimu wa Kipupwe, na
kwasababu hiyo, vipindi vya upepo wa Kusi baharini vinaweza kuanza kujitokeza
na kuambatana na mawimbi makubwa kwa baadhi ya nyakati.
Imetolewa na: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
No comments:
Post a Comment