TEN/MET YACHANGIA MILIONI 12 KWA SHULE TATU ZA MSINGI MOROGORO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 2 May 2023

TEN/MET YACHANGIA MILIONI 12 KWA SHULE TATU ZA MSINGI MOROGORO

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mheshimiwa Fatma Mwasa (kushoto) akipokea taarifa ya jumla ya Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yaliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Mvuha, mkoani Morogoro, kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Ms. Faraja Nyalandu.

Mkuu wa Miradi, Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Ms. Martha Makala (kushoto mwenye kipaza sauti) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mheshimiwa Fatma Mwasa (kulia) namna mtandao huo unavyofanya kazi alipotembelea Banda la TEN/MET kwenye kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa hivi karibuni yaliofanyika Shule ya Msingi Mvuha, mkoani Morogoro.

Wadau wa elimu wakiwa katika mikutano na kujadiliana na makundi ya wanafunzi, kamati na bodi za shule, wazee maarufu na viongozi wa dini, walimu, na wazazi ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro.

Wadau wa elimu wakiwa katika mikutano na kujadiliana na makundi ya wanafunzi, kamati na bodi za shule, wazee maarufu na viongozi wa dini, walimu, na wazazi ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro.

Wadau wa elimu wakiwa katika mikutano na kujadiliana na makundi ya wanafunzi, kamati na bodi za shule, wazee maarufu na viongozi wa dini, walimu, na wazazi ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro.

Wadau wa elimu wakiwa katika mikutano na makundi ya wanafunzi, kamati na bodi za shule, wazee maarufu na viongozi wa dini, walimu, na wazazi ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani Morogoro.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mheshimiwa Fatma Mwasa (kushoto) akimkabidhi zawadi mmoja wa wanafunzi wanaofanya vizuri darasani kwenye kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yaliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Mvuha, mkoani Morogoro, katikati anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Ms. Faraja Nyalandu.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Ms. Faraja Nyalandu (kulia) akitoa hotuba kwenye kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yaliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Mvuha, mkoani Morogoro, katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mheshimiwa Fatma Mwasa aliyekuwa mgeni rasmi.

Na Joachim Mushi, Morogoro

MTANDAO wa Elimu Tanzania (TEN/MET), umechangia jumla ya shilingi million 12 kwenye shule tatu za msingi zilizopo wilayani Morogoro, ikiwa ni kusaidia kutatua changamoto anuai ikiwemo kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwenye shule hizo.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Ms. Faraja Nyalandu hivi karibuni mkoani Morogoro kwenye hafla ya ufungaji wa Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayofanyika katika Kata ya Mvuha mkoani humo.

Akifafanua juu ya uchangiaji huo, Mwenyekiti wa Bodi ya TEN/MET, Ms. Nyalandu alisema shilingi million nne zitakwenda kusaidia ujenzi wa vyoo vya walimu Shule ya Msingi Bonye, shilingi Milion nne zingine zitasaidia ujenzi wa sakafu Shule ya Msingi Njianne na huku shilingi million nne zitachangia kwenye ununuzi wa madawati katika Shule ya Msingi Duthumi.

Katika maadhimisho ya Juma la Elimu kwa mwaka huu washiriki walipata fursa ya kushiriki kazi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa bweni la wasichana wenye ulemavu katika Shule ya Msingi Mvuha, kutembelea shule mbalimbali za msingi na sekondari ikiwemo Shule ya Msingi Njia nne, Duthumi, Bonye, na Magogoni huku Shule za Sekondari zilizotembelewa zikiwa ni pamoja na Bwakira Chini na Selembali.

Katika ziara hiyo washiriki walipata fursa ya kukutana na kujadiliana na makundi ya wanafunzi wa kike na kiume, kamati na bodi za shule, wazee maarufu na viongozi wa dini, walimu, na wazazi huku lengo la majadiliano hayo ikiwa ni kutoa hamasa katika jamii ili kuboresha huduma za utoaji wa jamii kwa kupata mafanikio na kuibua changamoto zinazowakabili na kutoa mapendekezo ya namna ya kuzitatua. 


No comments:

Post a Comment