Na Adeladius Makwega-MWANZA
MKUFUNZI Atanas Muechela wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya amesema kuwa mchezo wa Netiboli ni mchezo unaongoza kuliletea taifa la Tanzania tuzo, medali. nishati kadhaa na zinalipa sifa kubwa taifa letu kimataifa kuliko mchezo wowote, hivyo amehimiza Watanzania kujifunza, kuucheza na kuupenda mchezo huo.
Hayo yamesemwa kandoni mwa uwanja wa Netiboli katika mafunzo kwa Wakurufunzi wake wa kozi ya Astashahada ya Michezo chuoni hapo, Mei 9, 2023 Malya-Kwimba mkoani Mwanza.
“Kwa hakika mafanikio ya mchezo wa Netiboli ni makubwa mno, huku mwaka 2010 ikishiriki mashindano ya dunia ikiondolewa na Indonesia, ukiorodhesha utajaza kurasa na karatasi nyingi. Mafanikio yake si ya kuyatafuta kwa tochi, Timu yetu ya Taifa ya Netiboli- Taifa Queens inafanya vizuri, inajulikana na kutambulika ulimwenguni kote, sasa jukumu lililobakia ni uhamasishaji zaidi kufanyike.”
Akifundisha mchezo huo kwa wakurufunzi wake 54, Mkufunzi Muechela aliwaelekeza namna ya kutupa mpira kwa kutumia njia tatu; kutokea kifuani (Chest Pass), kutokea juu (Overhead Pass) na kutupa mpira kwa kudunda (Baunce Pass)
Akiendelea kufundisha mchezo huo, wakurufunzi wake walipewa nafasi mbalimbali kama vile za kusimamia mafunzo hayo kama wakufunzi kulingana na alivyoelekeza darasani, nafasi hiyo katika darasa hilo lililodumu kwa dakika 90 alipewa Hamisi Phares Meleki ambaye naye anasoma Astashahada hiyo ya Michezo, alisimamia vizuri huku akiuliza kama hakukutokea mkurufunzi hata mmoja aliyeumia mchezoni, majibu yalikuwa wote walikuwa salama, akisisitiza kuboreshwa namna walivyoucheza mchezo huu.
Wakati wakuhitimisha somo hilo mkurufunzi Raham Simba akiwa miongoni mwa wanachuo hao alitoa tathmini hii,
“Hapa nimebaini tunavyoucheza mchezo huu tuna uwezo tofauti tafauti, kama yupo mwezetu ambaye unabaini hawezi kufanya vizuri baadhi ya mazoezi, nawaombeni msisite kumsaidia, hata kama ni mimi, tujitume na tusiogope kuelekezana, hapa umekosea hili na lile na unatakiwa kufanya hivi.”
Mchezo wa Netiboli ambao pia hufahamika kama Mpira wa Pete jina ambao linakataliwa na baadhi yao huchezwa sana na wanawake huku waanzilishi wa michezo huu walikuwa Waingereza mwaka 1890, huchezwa na timu mbili na kila timu huwa na wachezaji saba. Wachezaji hao hujulikana kama GK(Goal Keeper),GS(Goal Shooter),WD (Wing Defense), GD (Goal Defense),WA (Wing Attack), GA(Goal Attack),C(Center) hizo zikiwa pia nafasi za wachezaji kwa kila timu.
No comments:
Post a Comment