Wananchi viziwani Zanzibar wakiendelea kupata huduma mbalimbali baada ya uzinduzi wa kampeni ya Umebima. |
Sehemu ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya Umebima visiwani Zanzibar. |
BENKI ya NMB ikiwa wasambazaji wa bidhaa mbalimbali za
makampuni 10 ya bima, wamezindua rasmi kampeni ya 'Umebima - Teleza na Hii!'
visiwani Zanzibar itakayowawezesha kutoa elimu na kuhamasisha mauzo ya bima
mbalimbali zikiwemo za: Majanga, afya, moto, machinga, maisha, vikundi, vyombo
vya moto, nyumba, biashara, kilimo, usafirishaji na kadhalika, zitakazosaidia
kutoa fidia endapo majanga yatatokea.
Kampeni hii imezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi
- Idrissa Kitwana Mustafa na Mkuu wetu wa Idara ya Bima wa NMB - Martine
Massawe, huku Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Rashid Simai Msaraka na Meneja wa
Biashara wa NMB Zanzibar - Naima Said Shaame wakishuhudia.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi Bw.
Idrissa Kitwana Mustafa aliwaasa wananchi kuchukua juhudi ya kuzielewa
aina zitolewazo za bima, ili waweze kukata kwani ni kwa manufaa yao ya sasa na
hata baadae.
Lakini pia, aliiipongeza NMB kwa ubunifu wa kampeni hii ambayo
ni fursa nzuri ya maendeleo.
Aidha, Mkuu wa Idara ya Bima wa benki hiyo, Bw.
Martine Massawe, alisema timu ya NMB itakua mitaa mbalimbali visiwani Zanzibar
kwa mwezi mzima kuhakisha wanatoa elimu ya bima na wanananchi wanaelewa ili
waweze kuchagua ni ipi wanaihitaji. Bima hizi, mteja wa NMB na asiyekua mteja
anaweza kuzinunua kutoka kwa matawi ya benki hiyo yaliyotapakaa nchi nzima.
No comments:
Post a Comment