BEST BRAND DISTRIBUTOR YADHAMIRIA KUZALISHA AJIRA KWA VIJANA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 9 February 2023

BEST BRAND DISTRIBUTOR YADHAMIRIA KUZALISHA AJIRA KWA VIJANA

Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto akizungumza na wanahabari.

Mkurugenzi kampuni ya Best Brand Distributer.

Na Dunstan Mhilu

KAMPUNI ya Best Brand Distributor imesema imedhamiria kuzalisha ajira kwa vijana wa kitanzania na kuingizia serikali mapato kupiitia uuzaji wa bidhaa zake zinazozalishwa na Kampuni ya Relaxo yenye Makao Makuu yake Makuu nchini India.

Hayo yalizungumzwa na Mkurugenzi wa Duka la Viatu vya Kampuni ya Relaxo, Khalid Mbarak Salim alipofanya mahojiano na HabariLEO na kusema kuwa wamedhamiria kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya biashara ili kuwapatia vijana wakitanzania ajira za kudumu.

“Kutokana na mazingira mazuri yaliyowekwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan tumeamua kumuunga mkono Rais kwakufungua maduka mengi nchini ili tutoe ajira kwa vijana wetu ncchini kwakuwa Kampuni yao ni mshirika na wakala mkubwa wa Kampuni ya Kimataifa ya nchini India inayotengeneza bidhaa za Flite na Sparks ambavyo ni viatu, mabeki vifaa vya michezo na nyinginezo nyingi ukifika dukani kwetu utazifahamu na bei zetu ni nafuu” alisema Salim

Katika muktadha wa kuongeza ajira kwa vijana ambapo duka hilo limeajiri vijana wa kitanzania 5, alisema Kampuni inampango wa kufungua maduka 20 yakayotapakaaa katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ambayo yataongeza idadi ya waajiriwa na kulipatia Taifa mapato yake.

Kadhalika upo mpango wakujenga kiwanda kikubwa cha uzalishaji wa bidhaa za Relaxo kwakuwa wameingia ubia na kampuni ya Relaxo, kiwanda hicho kitazalisha bidhaa kwa ukanda mzima wa Afrika Mashariki na kitajengwa Tanzania.

“Nikisema tumedhamiria kumuuunga mkono Rais Samia namaanisha, tutao ajira nyingi hapa nchini, tutalipa kodi kwa wakati ili kuhakikisha uchumi wa nchi yetu unakuwa na kuimarika zaidi,”

Hata hivyo Salim anaiomba serikali kuruhusu wafanyabiashara nchini kufanya biashara zao masaa 24 ili kuwapa fursa wafanyakazi ambao huchelewa kutoka kazini na amabo pia huingia kazini alfajiri na hivyo kukosa muda wakufanya manunuzi.

“Hili litaleta tija kwetu tukkiamini tutauza ziadi na tutapata faida kubwa ambayo itasaidia kuchangia kiasi kikubwa cha kodi serikalini,” alisema.

No comments:

Post a Comment