Kaimu Meneja wa Usajili wa Bidhaa na Majengo TBS Gwantwa Samson Mwakipesile akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu taratibu za kusajili bidhaa na vipodozi kwa wafanyabiashara mbalimbal nchini.
Afisa Udhibiti Ubora TBS ambaye anashughulika na usajili wa bidhaa za vipodozi vinavyotoka nje ya nchi Mbuni Mwampeta akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam
NA MUSSA KHALID
SHIRIKA la Viwango nchini Tanzania -TBS limewataka
watanzania wanaotaka kufanyabiashara ya chakula na vipodozi nchini kuhakikisha
wanajisajili mapema ili kuweza kuwalinda wananchi waepukane na madhara
yanayoweza kujitokeza.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam
na Kaimu Meneja wa Usajili wa Bidhaa na Majengo TBS Gwantwa Samson Mwakipesile wakati
akizungumzia taratibu za kusajili bidhaa na
vipodozi kwa wafanyabiashara mbalimbal nchini.
Mwakipesile amesema kuwa licha ya Shirika hilo
kuwezesha biashara mbalimbali pia linajukumu la kuwalinda watanzania ambao
wanatumia bidhaa hizo za vyakula na vipodozi.
Amesema
lengo la kufanya usajili wa bidhaa na majengo ni kujiridhisha kabla ya kuruhusu
majengo kutumika kuhifadhi bidhaa za vipodozi na chakula kwamba yanakidhi
vigezo vilivyowekwa ambavyo vitafanya bidhaa zinazotunzwa kwenye majengo hayo
ziendelee kuwa bora na salama kwaajili ya matumzi.
‘Suala
la usajili ni takwa la Kisheria limewekwa kwa mujibu wa sheria kwani sheria ya
viwango inasema kwamba mtu yeyetoe haruhusiwi kuuza bidhaa ya chakula wala
kipodozi kabla haijasajiliwa hivyo kwa kuwa ni takwa la kisheria
wafanyabiashara wote wanapaswa kufanya hivyo’amesema Mwakipesile
Kwa upande wake Afisa Udhibiti Ubora TBS ambaye
anashughulika na usajili wa bidhaa za vipodozi
vinavyotoka nje ya nchi Mbuni Mwampeta amesema mbinu wanazozitumia katika
usajili ni kuangalia ubora kwa kupeleka bidhaa hizo maabara lakini pia kuangalia viambata vilivyotumika kwenye
utengenezaji.
Aidha akielezea kuhusu madhara anyaoweza kupata mtu
pindi anapotumia vipodozi vyenye viambata sumu ni pamoja na kuwa na wekundu na
weusi kwenye ngozi pamoja na kupata muwasho.
No comments:
Post a Comment