VITA DHIDI YA UKATILI VINAHITAJI KUJITOA ZAIDI KULIKO FEDHA: WAZIRI DKT. GWAJIMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 25 May 2022

VITA DHIDI YA UKATILI VINAHITAJI KUJITOA ZAIDI KULIKO FEDHA: WAZIRI DKT. GWAJIMA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akifungua Mkutano wa wadau wanaotekeleza Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) Mkoa wa Dar es Salaam Mei 25, 2022.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima akikabidhi Cheti cha pongezi kwa Mkaguzi Msaidi wa Polisi Devotha Sanga kwa jitihada zake anazochukua katika kukabiliana na ukatili kwenye eneo lake la kazi wakati wa Mkutano wa wadau wanaotekeleza Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) Mkoa wa Dar es Salaam Mei 25, 2022 katika Ukumbi wa Karemjee.

Na MJJWM Dar Es Salaam

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima, amezitaka Kamati za Ulinzi wa Wanawakena Watoto (MTAKUWWA ) Mkoa wa Dar es Salaam  kubuni mbinu za kukabiliana na vitendo ya ukatili kwenye  jamii ili kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kwaani vita hivyo vinahitaji zaidi kujtoa kuliko fedha.

Dk. Gwajima ameyasema hayo Mei 25, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa Kamati hiyo wenye lengo la kuweka mikakati ya kukabili vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ndani ya Jamii. Waziri Dkt  Gwajima alisema Serikali imekuwa ikijitahidi kuhakikisha inawezesha mikakati yote ya kulinda Wanawake na watoto dhidi ya vitendo vya ukatili.

"Katika mkutano wenu huu, hakikisheni mnakuja na jibu ambalo litasaidi Kamati zenu za MTAKUWWA, kufanikiwa katika vita hii ya kupambana na ukatili," alisema Waziri  Dkt. Gwajima.

Waziri Dkt.Gwajima amefafanua kuwa, hatua hiyo itasaidia kuwa na taifa bora la baadaye, huku akifafanua bado hali si nzuri, hasa kutokana na watoto wanaozura mitaani.

"Watoto wamekuwa wakidandia magari kutoka vijijini na kukimbilia mijini na kujikuta wakilala katika vituo vya mabasi na wengine chini ya madaraja, hali hii si nzuri, tunatengeneza taifa baya la baadaye," alisema.

Akifafanua kuwa Kamati za MTAKUWWA zinatakiwa, kufuatilia changamoto za watoto, kujua idadi yao kuanzia kwenye vitongoji hadi vijiji na kuzifanyia kazi haraka iwezakavyo kabla hawajakimbia kwenda mijini na kuishia mitaani.

"Lakini pia wanaume wanaotelekeza watoto wao waache tabia hiyo, kwani lengo la serkali ni kujenga taifa bora, hivyo kila mmoja Wetu ahakikishe anasimamia malezi Bora ya familia yake," alisema Waziri Dkt Gwajima.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Zainab Chaula, ameonesha kukerwa na jina la Watoto wa mitaani na kufafanua kuwa hakuna mtoto wa mtaani bali kila mmoja ana mzazi wake.

"Acheni kutumia jina hilo,  hao watoto Wana wazazi wao, hivyo ni.muhimu kuwatambua na kuwasaidia waondokane na maisha hayo," alisema Dk. Chaula.

Naye Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chang'ombe (OCD)  SSP Ariziki Makwaya, alisema Kuna haja ya kuwa na nyumba salama nyingi ili kusaidia manusura wa vitendo vya ukatili.

Alisema, manusura anapofika au kufikishwa Kituo cha Polisi anatakiwa asirudi maeneo hatarishi, na kwamba wanalazimika kurudi huko kutokana na ukosefu wa nyumba salama.

"Huo ndio ushauri wangu mheshimiwa waziri, kwamba tuwe na nyumba salama nyingi ili kusaidia manusura wa vitendo vya ukatili," alisema SSP Makwaya.

No comments:

Post a Comment