RAIS SAMIA HASSAN AFUNGUA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 23 February 2022

RAIS SAMIA HASSAN AFUNGUA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE

 

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisogeza kitambaa kama ishara ya ufunguzi rasmi wa Shule ya uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kibaha Mkoani Pwani  leo tarehe 23 Februari, 2022.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza mratibu wa mradi wa Chuo Bi. Emmanuela Kaganda kuhusu maeneo mbalimbali ya ndani ya Shule hiyo Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kibaha Mkoani Pwani mara baada ya ufunguzi wake leo tarehe 23 Februari, 2022.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi wa Vyama vya Siasa kutoka nchi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere  Kibaha Mkoani Pwani  leo tarehe 23 Februari, 2022.



Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea kukagua maeneo mbalimbali ya Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Kibaha Mkoani Pwani mara baada ya kukifungua rasmi leo tarehe 23 Februari, 2022.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi cheti cha mafunzo ya muda mfupi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima katika sherehe za ufunguzi wa  Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Kibaha Mkoani Pwani leo tarehe 23 Februari, 2022.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akizungumza na Viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, Wananchama wa CCM pamoja na Wananchi wa mkoa wa Pwani mara baada ya kufungua Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Kibaha Mkoani Pwani leo tarehe 23 Februari, 2022.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Kibaha mkoani Pwani  leo tarehe 23 Februari, 2022.

No comments:

Post a Comment