Waziri wa Ujenzi na
Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa (kulia), mara baada ya kupokea mabehewa
44 ya yatakayotumika katika reli ya kati. |
Muonekano wa behewa litakalotumika kusafirisha mizigo katika reli ya kati, kati ya Dar es Salaam hadi Isaka. |
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na watumishi wa TPA na TRC mara baada ya kupokea mabehewa 44 yatakayotumika katika reli ya kati. |
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa mkandarasi SUMA JKT anayejenga Bandari Kavu ya Kwala iliyopo Ruvu, mkoani Pwani. |
WAZIRI
wa
Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ametoa miezi sita kwa Mamlaka ya Usimamizi
wa Bandari nchini (TPA), kuhakikisha ujenzi wa Bandari Kavu ya Kwala iliyopo
Ruvu mkoani Pwani unakamilika.
Akikagua maendeleo ya
Ujenzi wa mradi huo ambao ulianza kujengwa tangu mwaka 2017, Profesa Mbarawa
ameelezea kutokuridhishwa kwake na maendeleo ya mradi.
"...Sijaridhika
na kasi ya ujenzi wa mradi huu hivyo nawataka TPA na SUMA JKT katika kipindi
cha miezi sita ijayo kazi hii iwe imekamilika na nitakuwa nikija kila mwezi
kukagua maendeleo ya mradi," alisema Profesa Mbarawa.
Profesa Mbarawa
ameagiza mkataba wa ujenzi wa mradi huo urekebishwe, TPA wamlipe mkandarasi kwa
wakati na kutafuta vifaa vinavyohitajika katika mradi kama saruji, kamera za
usalama na kuhakikisha bei za vifaa zinaendana na soko.
Naye Mkurugenzi Mkuu
wa TPA, Bw. Erick Hamis amemhakikishia Prof. Mbarawa kuwa mradi huo utakamilika
katika kipindi cha miezi sita kama alivyoagiza ili kupunguza msongamano katika
Bandari ya Dar es Salaam na kuiwezesha kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.
“Sisi TPA tunaihitaji
sana Bandari hii kwani itatupunguzia msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam
na kutoongezea nafasi ya kuhifadhi mizigo mingi zaidi, na hivyo kuongeza
mapato.
Zaidi ya makontena
3,400 yanatarajiwa kuhifadhiwa katika Bandari Kavu ya Kwala itakapokamilika.
Kwa upande wake
Msimamizi Mkuu wa Mradi huo, Kanali Samwel Machemba kutoka SUMA JKT ameahidi kukamilisha
ujenzi huo kwa wakati.
Katika hatua nyingine
Waziri wa Ujenzi, Prof. Mbarawa amepokea mabehewa 44 yatakayotumika katika
Shirika la Reli nchini, TRC na kuwataka viongozi na madereva watakao yaendesha
kuhakikisha yanatunzwa vizuri ili yaweze kudumu kwa muda mrefu.
"...Tutaendelea kutoa
fedha kwenye reli ya kati na SGR hivyo kazi yenu iwe kulinda miundombinu na
kukusanya fedha," amesisitiza Profesa Mbarawa.
Aidha amezitaka
taasisi zote zilizo chini ya wizara yake kufanya kazi kufikia malengo na zile
zinazokusanya mapato msisitizo uwe kukusanya mapato.
Mapokezi ya mabehewa
44 ni sehemu ya mchakato wa uboreshaji wa reli ya kati, kati ya Dar es Salaam
hadi Isaka, ambapo tayari ujenzi wa njia ya reli na madaraja umeimarishwa,
ufufuaji wa vichwa vya treni na ukarabati wa mabahewa na injini za treni
unaendelea.
Imetolewa
na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.
No comments:
Post a Comment