TOENI MAJAWABU YA CHANGAMOTO ZA WATOTO - DK. JINGU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 11 November 2020

TOENI MAJAWABU YA CHANGAMOTO ZA WATOTO - DK. JINGU


Katibu wa Jukwaa la wahariri nchini Neville Meena akimueleza Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii (Hayupo pichani) maandalizi ya utoaji wa tuzo kwa Waandishi wa Habari zinazotarajiwa kutolewa mwezi Desemba mwaka huu. Kulia ni Mjumbe wa Jukwaa hilo Lilian Timbuka.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akizungumza na timu ya Jukwaa la Wahariri nchini ofisini kwake kuhusu uandishi wa Habari za watoto na Tuzo wa waandishi wa Habari za watoto zinarakazofanyika Desemba.

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Dk. John Jingu amewataka waandishi wa Habari nchini kutafiti na kuainisha masuala mbalimbali yanayohusu watoto ili kujenga Jamii yenye mtazamo chanya. 

Dk. JINGU metoa kauli hiyo katika mkutano wake na Ujumbe kutoka Jukwaa la Wahariri nchini TEF uliofika Ofisini kwake kutambulisha maandalizi ya tuzo za Waandishi wa Habari kuhusu watoto watoto kwa mwaka 2019 zinazotarajiwa kufanyika mwezi Desemba, 2020.

 

Amesema waandishi wa habari ni muhimu kuandika habari zinazoijenga Jamii na kutafuta changamoto zinazowahusu watoto badala ya kujikita katika ukosoaji pekee.

 

Ameongeza kuwa waandishi wa habari ni wadau muhimu wa kuleta mabadiliko hivyo waandike habari zenye majawabu kwenye jamii ili zisilete athari hasa kwa watoto waliofanyiwa ukatili.

 

"Wakati mwingine mwandishi anaibua tatizo halafu anawaacha hewani kumbe na yeye ni mdau anatakiwa kutoa mchango wa kutafuta jawabu. Tukiwa na waandishi wenye majawabu watatusaidia sana," amesema Jingu.

 

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deodatus Balile amesema Tuzo za Waandishi wa Habari hususani Habari za Watoto zinaangalia zaidi uandishi wa habari za watoto wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali kwa kushirikiana na Serikali ili kupata suluhisho la pamoja kwa Ustawi wa Jamii nzima.

 

Naye Katibu wa Jukwaa hilo, Neville Meena ameelezea kuwa katika maandalizi ya tuzo hizo watashirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii kwa kuwa ndiyo Wizara yenye dhamana na masuala ya maendeleo na ustawi wa watoto.

 

Katika hatua nyingine, Dk. Jingu amewahimiza waandishi wa habari katika maeneo mbalimbali nchini kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Haki ya Mtoto itakayofanyika tarehe 20 Desemba 2020.

 

Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni 'Dunia salama kwa kila Mtoto inawezekana; Chukua hatua'.

No comments:

Post a Comment