MFAHAMU MWANAMKE MWEUSI ALIYECHANGIA USHINDI WA BIDEN....! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 11 November 2020

MFAHAMU MWANAMKE MWEUSI ALIYECHANGIA USHINDI WA BIDEN....!

Bi. Kamala Harris.

KAMALA Harris ataweka historia atakapokuwa makamu rais wa kwanza hapo Januari - lakini mwanamke mwingine mweusi alikuwa na jukumu muhimu katika kuhakikisha Biden na Harris wanajinyakulia nafasi ya kuingia Ikulu.

Wakati anasherehekea kupata ushindi pamoja na Joe Biden, Harris mwanamke wa kwanza mweusi mwenye asili ya Asia kuwa makamu wa rais mteuliwa alihakikisha ametambua kundi fulani kwa kuchangia sehemu kubwa ya kufanikiwa katika kampeni yake.

Seneta Harris alitambua kundi la wanawake walio wachache - hasa wanawake weusi - ambao mara nyingi hukosa kutambuliwa lakini pia wamedhihirisha kuwa ni muhimili wa demokrasia yetu.

Wakiwa nyumbani nje tu ya eneo la Atlanta, Georgia wanafamilia hao walikuwa wana bubujikwa na machozi wakitazama hotuba ya Bi. Harris.

"Georgia sasa ni bluu, chama ambacho ni chachu ya mabadiliko ya maisha katika jimbo na wakazi wake, hasa raia weusi wanaoishi hapa," amesema Kristin Hunt, 27.

"Yote haya ni kwasababu ya Stacey Abrams na wanawake wengine wengi weusi walio hapa na hata katika mashirika ya vijijini kusajili watu kupiga kura na kudhihirisha kwanini kura zetu ni muhimu."

Safari ya Joe Biden ya kuelekea Ikulu imeungwa mkono kwa kiasi kikubwa na rais weusi wenye asili ya Marekani.

Wapigaji kura weusi ndio waliokuwa na mchango mkubwa katika ushindi wa Biden Kusini mwa Carolina na kupelekea kuchaguliwa kama mgombea wa chama.

Pia alishinda Pennsylvania - wakati wa uchaguzi - mchango mkubwa ukitokea kwa wapiga kura weusi katika miji kama vile Philadelphia na Pittsburgh.

Karibu wapiga kura 9 kati ya 10 weusi walipiga kura ya kuchagua chama cha Democrat, kulingana na kura za maoni ingawa Donald Trump aliongeza idadi ya kura alizopata ikilinganishwa na mwaka 2016.

Lakini unapouliza ni nani hasa katika miji hiyo aliyemsaidia Biden kushinda uchaguzi, wengi watasema ni wanawake weusi katika jamii zao.

Wanawake kama vile Kruzshander Scott, mwandalizi huko Jacksonville, Florida, aliyeniambia kwamba amepokea vitisho na kupewa ulinzi zaidi wiki za mwisho za uchaguzi wakati anaendeleza harakati zake za kuhakikisha wapiga kura weusi wanajitokeza kwa wingi kuliko uchaguzi mwingine wowote ule katika historia.....

-BBC

No comments:

Post a Comment