Sehemu ya wajasiriamali wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa kinga kwa ajili ya kuendeleza Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa homa kali ya mapafu Covid 19 |
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Kwa muktadha huo akawataka wajasiriamali wa mkoa wa Arusha chini ya Sido kutumia malighafi zetu za ndani na utaalamu wetu wa ndani katika kupambana na maambukizi ya Ugonjwa wa homa kali ya mapafu Covid 19 unasababishwa na virusi vya korona kwa kuwa janga hili linatupa ya Sote
Kwitega aliyasema hayo wakati akipokea vitakasa mikono sabuni na barakoa zilizotengenezwa na wajasiriamali wa mkoa wa Arusha wanaofanyakazi chini ya Sido kwenye hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Alisema kwa wajasiriamali hao wameonyesha muitikio wa kauli ya mh.Rais wa kutumia ubunifu wetu wa ndani wa kutengeneza bidhaa zao kwa kutumia malighafi zetu za ndani kuwezesha watanzania kuweza kujikinga na Ugonjwa wa Covid 19 bila kutumia gharama kubwa ya kununua bidhaa hizo.
"Mmetuonyesha kwa vitendo kuwa bidhaa hizi ambazo zinauzwa kwa bei elekezi ya serikali kwa ujazo wa mml40 kwa bei ya tsh.2000 badala ya tshs.3000 jambo hilo litasaidia watanzania wengi kuweza kujikinga na Ugonjwa huu"alisema Kwitega
Kwa Upande wake Meneja wa Sido Mkoa wa Arusha Nina Nchimbi alisema kuwa baada ya janga hili kutokea tuliona ni fursa kwa wajasiriamali kuweza kuzalisha bidhaa zenye viwango vinavyokubalika ili kuokoa watanzania na janga hili ndio maana leo tupo hapa kutambulisha bidhaa hizi.
Alisema kuwa Sido siku zote ipo kuwaonyesha njia wajasiriamali katika kutengeneza bidhaa zenye ubora unaokubalika sanjari na bidhaa zenye ubora wa hali ya juu ambazo zinapingana na maisha ya Mtanzania.
Awali akitoa taarifa mbele ya Karibu tawala wa mkoa wa Arusha Mwenyekiti wa Wajasiriamali waliochini ya Sido Yasin Bakary alisema bidhaa hizo ikiwemo Sabuni za maji Vitakasa mikono na Barakoa wanauza kwa bei inayowajali watanzania ikiwemo Barakoa kwa tshs.700 badala ya 3000 au 1000.
Alisema walipoona bidhaa zinazozalishwa nje ya nchi zimekuwa bei juu waliamua na kuona watumie bidhaa za ndani kuzalisha bidhaa za kujikinga na Ugonjwa wa Covid 19 ili kuwasaidia watanzania kwenye mapambano ya kujikinga na maambukizi ya Ugonjwa wa homa kali ya mapafu.
Nae Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt.Edson Sichalwe alisema kuwa wamejikita kutoa elimu kwa jamii kujikinga na Ugonjwa wa homa kali ya mapafu Covid 19 na kwa sasa wamejikita kwenye uvaaji wa barakoa
Akawataka kuunganisha nguvu kwani mapambano ya kujikinga na maambukizi ya Ugonjwa wa Covid 19 si ya wizara ya Afya pekee ni kwa kila mdau kushiriki ikiwemo hili la uzalishaji wa bidhaa za kujikinga kwa kuzalisha kwa wingi ili kumfikia mwananchi wa chini kwa bei ya chini anayoweza kuimudu.
No comments:
Post a Comment