Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo),
Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza hilo
akizungumza katika kikao kazi cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo
kilichofanyika Jijini Dodoma.
Katibu wa Baraza hilo Bw.Andrew
Ponda akisoma maazimio kwenye kikao kazi cha Baraza la Wafanyakazi wa
wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la
Wizara hiyo Bw.Stuart Mgunya,akizungumza kwenye kikao kazi cha Baraza
la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Jijini
Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na
Uvuvi(Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye pia ni mwenyekiti wa
baraza hilo akieleza jambo katika kikao kazi cha Baraza la Wafanyakazi
wa wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya
Utawala, Rasilimali Watu Sekta ya Mifugo Bi. Teddy Njau akizungumza
katika kikao kazi cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo
kilichofanyika Jijini Dodoma.
Mchumi kutoka wizara ya mifugo
Bw.Francis Makusaro akitoa taarifa kwenye kikao kazi cha Baraza la
Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Jijini
Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na
Uvuvi(Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye pia ni mwenyekiti wa
baraza hilo akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kikao kazi cha
Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Jijini
Dodoma.
Na.Mwandishi wetu,
Dodoma
BARAZA la Wafanyakazi Wizara ya
Mifugo na Uvuvi Sekta ya Mifugo limeazimia kuwatetea wafugaji ili
kutovunja sheria,kanuni na kuwa fanya kutambua haki zao katika
kutimiza malengo katika shughuli zao.
Azimio hilo limetolewa leo na
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo), Prof. Elisante Ole
Gabriel ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza hilo katika kikao kazi cha
Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Jijini
Dodoma.
Prof. Gabriel amesema kuwa sekta
hiyo imejipanga vema kuchangia katika uchumi wa viwanda kwa kuzalisha
malighafi ya kutosha itakayotumika katika viwanda vya hapa nchini
katika kusukuma uchumi wa kati.
"Watumishi wote wa sekta hii
mnatakiwa kufanya kazi bila uzembe na kutoleta ubadhilifu katika sekta
hii ili kulinda weledi wenu" amesema
Prof.
Gabriel.
Aidha katika kikao hicho
Prof.Gabriel ameeleza kuwa wameazimia kutekeleza majukumu ya wizara
katika kiwango bora kinacho hitajika ili kuleta ubora katika
kuwahudumia wananchi.
Prof. Gbriel ameweka wazi kuwa
kila mfanyakazi katika sekta hiyo atakatwa kiasi cha shillingi
10,000/= ili kuweza kuchangia katika mfuko wa faraja unaosaidia katika
matatizo mbalimbali yanayomkuta mfanyakazi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
TUGHE Tawi la Wizara hiyo Stuart Mgunya amesema kuwa wafanyakazi
wanahaja ya kuwa pamoja katika kuboresha ustawi wa watumishi ili
kufikia malengo yao katika kutimiza majukum
yao.
Mgunya ametoa wito kuwa
kupatikane siku moja ya kuweza kuwashika mkono wastaafu katika wizara
hiyo ikiwa ni ishara ya shukrani na pongezi kwa utumishi wao ulio
tukuka katika kutumikia taifa.
Naye Kaimu Mkurugenzi Idara ya
Utawala, Rasilimali Watu Sekta ya Mifugo Teddy Njau amesema sasa
ni wakati muhimu watumishi kujiunga katika mfuko wa faraja wenye lengo
wa kusaidiana katika wizara hiyo.
Katika kikao hicho baraza hilo
limemchagua Andrew Ponda kuwa Katibu wa Baraza na Katibu Msaidizi ni
Suzanna Silayo ambao watakuwa madarakani kwa miaka
mitatu.
No comments:
Post a Comment