MAAMBUKIZI UGONJWA WA CORONA YAFIKIA 480 TANZANIA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 29 April 2020

MAAMBUKIZI UGONJWA WA CORONA YAFIKIA 480 TANZANIA

 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkbidhi gari la kubebea wagonjwa Mbunge wa Urambo, Margaret Sitta wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa kwa wabunge yenye thamani ya shilingi bilioni 6. Katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akishudia.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa na baadhi ya wabunge waliokabidhiwa  funguo  za magari ya kubebea wagonjwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 29, 2020. Magari 50 ya kubebea wagonjwa yenye thamani ya shilingi bilioni 6 yalikabidhiwa kwa wabunge.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa  kwa wabunge yenye thamani ya  shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na wa tatu kulia ni Mbunge wa Nyasa ambaye pia ni  Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi, Stella Manyanya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa  kwa wabunge yenye thamani ya  shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Dodoma

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametoa taarifa ya mwenendo wa Ugonjwa wa Corona nchini, ambapo amesema kuna maambukizi mapya ya ugonjwa huo kwa watanzania 196 ambapo kati yao; kutoka Bara ni 174, Zanzibar 22 na kufanya jumla ya watu waliopata maambukizi kuwa ni 480. 

Aidha,Waziri Majaliwa amesema kuwa idadi ya wagonjwa waliopona imeongezeka kutoka 48 hadi kufikia 167, (Zanzibar wako 36, Bara ni 83). 

Hali kadhalika vifo 6 vimetokea na kufanya jumla ya waliofariki kwa ugonjwa wa Corona kufikia 16 hadi sasa. 

Waziri Mkuu ametoa rai kwa Watanzania kuacha kutoa taarifa za uzushi za vifo kuwa kila kifo kinachotokea hakisababishwi na Ugonjwa wa Corona.

No comments:

Post a Comment