IDADI YA WAGONJWA TANZANIA YAFIKA 147 BAADA YA WAGONJWA 53 ZAIDI KUKUTWA NA VIRUSI HIVYO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 17 April 2020

IDADI YA WAGONJWA TANZANIA YAFIKA 147 BAADA YA WAGONJWA 53 ZAIDI KUKUTWA NA VIRUSI HIVYO

waziri wa Afya Ummy Mwalimu

WIZARA YA AFYA
nchni Tanzania imethibitisha visa vipya 53 vya ugonjwa wa corona hatua inayoongeza idadi ya watu walioathirika na ugonjwa huo kufikia watu 147.
Katika taarifa iliotumwa kwa vyombo vya habari , waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kwamba wagonjwa wote ni raia wa Tanzania.
Idadi hiyo ni kubwa zaidi kutangazwa kwa siku moja katika taifa la Afrika mashariki tangu wagonjwa wa kwanza wa virusi hivyo kugunduliwa katika eneo hili.
Amesema kwamba miongoni mwa wagonjwa hao 38 wanatoka katika mkoa wa Dar es salaam, 10 katika Kisiwa cha Zanzibar , mmoja kutoka Kilimanjaro , 1 kutoka Mwanza , Pwani Mtu 1 na Kagera mtu 1.
''Munaweza kuona nimetoa takwimu kubwa sana lakini tumeamua tuseme ukweli kwa sababu Watanzania sasa lazima waelewe kuwa tunakabiliwa na changamoto kubwa." alisema waziri huyo.
Ameongezea kwamba Idadi ya watu waliopona ni 11 huku waliofariki wakiwa 5.
Vilevile amewataka Watanzania kuchukua tahadhari kubwa kujilinda dhidi ya ugonjwa wa Corona.
"Kama kuna mmoja alikuwa na shauku basi ni wakati afahamu Corona inaanza na wewe kujikinga na pia uwakinge wengine"
Aidha afisa huyo wa serikali amesema kwamba kuna watu wenye dalili za ugonjwa wa corona ambao wamekuwa wakienda kupata huduma za matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kutokana na hilo ametoa wito kwa hospitali hiyo kutopokea wagonjwa kama hao akisema kwamba Muhimbili ni hospitali kuu ya rufaa inayokabiliana na magonjwa mengine na badala yake akawataka wagonjwa hao kuripoti katika hospitali ya rufaa ya mkoa ya Amana mjini Dar es Salaam.
Idadi hiyo ni kubwa zaidi kutangazwa kwa siku moja katika taifa la Afrika mashariki tangu wagonjwa wa kwanza wa virusi hivyo kugunduliwa katika eneo hili.

No comments:

Post a Comment