Mkurugenzi wa Kiwanda cha maziwa ya Asas Ahmed Asas akizungumza na waandishi habari mara baada ya kumalizika kwa kikao cha wadau wa afya walipokuwa wakijadili kuhusu kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
SERIKALI ya wilaya ya Iringa
imeipongeza kampuni ya Asas kwa mikakati ambayo wanayo katika kuhakikisha
wanajilinda na maambukizi ya virusi vya Corona ambavyo vimekuwa tishio kwa
maisha ya binadamu.
Akizungumza kwenye kikao cha
wadau mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema mkakati ambao
wanaoutekeleza kwa kujilinda na virusi vya Corona kwa wafanyakazi wake.
"Nimeona wametenga chumba
maalumu kwa ajili ya kutoa huduma ya kwanza kwa wafanyakazi wake na tayari
ameshatoa mafunzo kwa wafanyakazi watatu kwa ajili ya kutoa huduma ya kwanza
kwa wale ndio watakaohisiwa wanamaambukizi ya virusi vya Corona"alisema
kasesela
Kasesela alisema kuwa kampuni
ya Asas imefanikiwa kutoa elimu ya maambukizi ya virusi vya Corona kupitia
vyombo vya habari na makundi mbalimbali hivyo ni mfano wa kuigwa.
Aliitaka kampuni ya Asas
kuendelea kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwa
wananchi wote wa wilaya ya Iringa ili kuokoa maisha yao katika kipindi hiki
kigumu
Kwa
upande wake mkurugenzi wa Kiwanda cha maziwa ya Asas Ahmed Asas alisema kuwa
wamekuwa wakitoa elimu juu ya maambukizi ya virusi vya corona kwa waandishi wa
habari,wafanyakazi wa kampuni ya Asas na taasisi binafsi kwa lengo la kuepuka
kuambukizwa virusi vya corona.
Ahmed
alisema kuwa kwenye kampuni ya Asas wamefanikiwa na kuwa na chumba maalumu kwa
ajiri ya wafanyakazi watao kuwa na dalili za maambukizi ya virusi vya corona na
wameganikiwa kutoa elimu kwa baadhi ya wafanyakazi kwa lengo la kuwa msaada kwa
wafanyakazi wengine.
"Sisi
tupo tayari kutoa elimu juu ya maambukizi ya virusi vya corona sehemu yeyeyo
ile kwa kushirikiana na serikali ya wilaya ya Iringa kama ambavyo yumeanza na
mkuu wa mkoa wa Iringa Richard kasesela" alisema Ahmed
No comments:
Post a Comment