- THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 14 February 2020


Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega akifungua mkutano wa wadau wa elimu ya ualimu


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,Dr.Ave Maria Semakafu  akifafanua jambo katika mkutano wa tathimini ya mradi wa TESP.

Picha ya Pamoja ya Viongozi na wadau wa elimu ya Ualimu nchini katika mkutano wa tathmini ya mradi wa TESP.

Na Ahmed Mahmoud,Arusha.

MKUU
wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameipongeza serikali ya Canada kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuboresha elimu ya ualimu nchini kwa kujenga miundombinu ya majengo,TEHAMA na vifaa vya kufundishia pamoja na mafunzo kwa walimu kupitia mradi wa (TESP).

Akisoma risala ya Mkuu wa Mkoa iliyosomwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega amepongeza mafanikio ya mradi huo wa elimu  unaolenga kukuza ubora wa elimu nchini kwa kuwaandaa walimu bora wataoleta matokeo makubwa kwenye sekta ya elimu nchini.

“Napongeza Uwekezaji wa Tanzania na Canada katika elimu ya ualimu ambayo  kuanzia kwenye miundombinu hadi mafunzo kwa ualimu kwani Elimu ni jiko la kupika wataalamu watakaotufikisha kweye ” Alisema Kwitega

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,Dr.Ave Maria Semakafu  amesema kuwa Mradi huo  wamekutana jijini Arusha kufanya tathmini ya utekelezaji wa mradi  wa TESP  kwasababu huu mradi umejikita katika kuboresha taaluma zaidi,mradi wa kuboresha miundombinu uko katika hatua za mwisho kukamisha.

Pia kuna fedha zinatolewa kwa ajili ya uendeshaji wa vyuo kitaaluma ,kuna fedha zinatolewa kwa ajilli ya wanafunzi.

Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,Dkt.Lyabwene Mtahambwa amesema kuwa Mafunzo ya ualimu ni nguzo muhimu katika kuboresha elimu nchini ,tunawaandaa walimu kwa ubora watakaoleta matokeo mazuri .

“Tunawapa mafunzo walimu wawe na upendo kwa wanafunzi na kufanya kazi kwa kujitoa bila kusukumwa ili kufikia mafanikio ya kitaaluma” Alisema Kamishna

No comments:

Post a Comment