RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA TABORA-KOGA MPANDA KM 342.9, AFUNGUA BARABARA YA STALIKE MPANDA KM 36.9 PAMOJA NA STAND YA MABASI YA MIZENGO PINDA MPANDA MKOANI KATAVI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 10 October 2019

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA TABORA-KOGA MPANDA KM 342.9, AFUNGUA BARABARA YA STALIKE MPANDA KM 36.9 PAMOJA NA STAND YA MABASI YA MIZENGO PINDA MPANDA MKOANI KATAVI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Tanzania Dkt. Alex Mubiru kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda 342.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kulia, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale wa kwanza kulia, Waziri wa Madini Doto Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe pamoja na viongozi wengine.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Tanzania Dkt. Alex Mubiru, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda 342.9 katika sherehe fupi zilizofanyika katika manispaa ya Mpanda mjini mkoani Katavi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wengine, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Stendi Kuu ya Mabasi Mizengo Pinda nje kidogo ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kufungua stendi hio ya mabasi.

Sehemu ya Barabara ya Mpanda –Stalike iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wakandarasi, Wahandisi Washauri wa miradi ya barabara ya Tabora-Koga-Mpanda 342.9 katika sherehe fupi zilizofanyika katika manispaa ya Mpanda mjini mkoani Katavi.

No comments:

Post a Comment