KAMANDA wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Jumanne Murilo amewahakikisha usalama wa pesa na mali zao wafanya biashara na kuwataka waendeshe biashara zao kwa uhuru. Akizungumza na wafanyabiashara katika Jukwaa la wafanyabiashara 'Business Club' amesema Jeshi la Polisi mkoani humo limejipanga na lipo imara kuhakikisha wanafanyabiashara hawasumbuliwi na wahalifu.
Aliwaomba wafanyabiashara mkoani hapa kuhakikisha wanatumia vyema jukwaa la 'Business Club' katika kuhakikisha wanakuza maradufu vipato vyao na kujenga uchumi imara wa nchi.
"Tumejipanga na tunapambana kuzuia uhalifu kabla haujatokea kuliko kukabiliana nao ukishatokea," Murilo alisema.
Alisema wafanyabiashara wasiwe na wasiwasi bali wahakikishe wanafanya biashara zao kwa uhuru kwa kuwa jeshi lake limejipanga vyema kuhakikisha hakuna masuala ya uhalifu.
Kwa upande wake,Mkuu wa Kitengo cha Biashara cha Benki ya NMB toka makao makuu, Donatus Richard alisema benki hiyo itaendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara kupitia ‘Business Club’. Alisema kupitia elimu watakazokuwa wanatoa kwa wafanyabiashara zitakuwa zikiwasaidia sana wafanyabiashara katika shughuli zao za kila siku.
Donatus aliongeza kuwa kwa sasa benki yao itaendelea kuwa karibu na wateja wao na alisema wataendelea kutoa mafunzo mbali mbali kwa wateja wao yakiwemo masuala ya masoko pamoja na kodi. Alisema semina zao pia zimewasaidia wateja wao kuwa karibu na wateja wenzao ambapo jambo linalodumisha uhusiano mwema katika ufanyaji biashara zao.
Alisema kwa sasa benki yao ipo katika mikakati ya kuwapeleka wafanyabiashara 10 nchini China kwajili ya kuwenda kujifunza mambo ya kibiashara katika tamasha la biashara litakalo fanyika nchini humo katika mwezi wa 10, mwaka huu.Mmoja ya wafanyabiashara,Kejja Misungwi alisema anaiomba benki ya NMB kuhakiksha wanaendelea kutoa semina za mara kwa mara kwa wateja wao jambo ambalo litawasaidia wateja kupata elimu za biashara zitakazowawesha upatakinaji wa faida katika biashara zao.
No comments:
Post a Comment