WAFANYABIASHARA 7000 MBAGALA KUNUFAIKA NA MRADI WA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA SOKONI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 21 February 2019

WAFANYABIASHARA 7000 MBAGALA KUNUFAIKA NA MRADI WA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA SOKONI

Naibu Balozi wa Uholanzi hapa nchini, Lianne Houben, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa kupinga ukatili wa kijinsia katika Soko la Mbagala Rangi Tatu na Kampochea yaliyopo wilayani Temeke Jijini Dar es Salaam jana. Mradi huo ambao unaendeshwa na Shirika la Equality for Growth (EfG), unajulikana  kama Mpe Riziki si Matusi.
 Wasanii wa Kikundi cha Nimujo wakiigiza igizo la kupinga ukatili wa kijinsia sokoni.

 Mfanyabiashara Mariam Rashid akitoa ushuhuda jinsi alivyopambana na ukatili wa kijinsia.

 Katubu wa Soko la Gezaulole lililopo Manispaa ya Ilala, Salum Yusuph Salum akizungumza kwenye uzinduzi huo.

 Wanawake wafanyabiashara katika masoko hayo wakiwa kwenye uzinduzi huo.

 Mtaalamu Mshauri wa Miradi wa EfG, Glory Blasio, akiwajibika.

 Mwezeshaji wa kisheria sokoni, Consolater Cleophas, akitoa ushuhuda kwenye hafla hiyo.

 Uzinduzi ukiendelea.

 Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita, akihutubia kwenye uzinduzi huo.

 Viongozi wa masoko wakiwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Soko la Kampochea, Hemed Njiwa, Mwenyekiti wa Soko la Mbagala Rangi Tatu, Mrisho Juma Mlyomi na Hanzuluni Kwemeye kutoka soko la Kampochea.

 Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita akiserebuka sanjari na  Naibu Balozi wa Uholanzi hapa nchini, Lianne Houben wakati wa uzinduzi huo.

 Hapa ni kuserebuka kwa kwenda mbele wakati wimbo wa wanawake na maendeleo ukipigwa.

 Wafanyakazi wa EfG waliojumuika kwenye uzinduzi huo.

 Mwezeshai wa kisheria masokoni, Aisha Juma akitoa ushuhuda.

 Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu, Shaban Othman, akizungumza kwa niaba ya Mgeni rasmi wa hafla hiyo Mbunge wa Mbagala, Issa Mangungu.

 Mfanyabiashara wa kuku katika Soko la Mbagala Rangi Tatu, Zainabu Mussa akizungumzia ukatili wa kijinsia katika soko lao.

 Mwenyekiti wa Soko la Mbagala Rangi Tatu, Mrisho Juma Mlyomi, akizungumza.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa EfG, Penina Reveta akizungumza.

Picha ya pamoja

Na Dotto Mwaibale

WAFANYABIASHARA 7000 katika Soko la Mbagala Rangitatu na Kampochea yaliyopo wilayani Temeke jijini Dar es Salaam kunufaika na mradi wa kupinga ukatili wa kijinsia katika masoko hayo ujulikanao kama Mpe Riziki si Matusi.

Mradi huo unaendeshwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Equality for Growth (EfG) kwa ufadhili wa Ubalozi wa Uholanzi hapa nchini ambao wametoa  shilingi milioni 34 ukiwa na lengo  la kuhakikisha wafanyabiashara hao wanajua haki zao na kuwa na mazingira  mazuri ya kufanyia biashara zao pasipo kuwepo na vitendo vyovyote vya ukatili wa kijinsia.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua mradi huo jijini Dar es Salaam juzi, Naibu Balozi wa Uholanzi hapa nchini, Lianne Houben alisema nchi yake itaendelea kufadhili miradi ya namna hiyo ili kuhakikisha wafanyabiashara wanafanya biashara zao kwenye mazingira rafiki.

"Tunaunga mkono juhudi zinazofanywa na EfG za kuwawekewa mazingira bora ya kufanyia biashara wafanyabiashara masokoni" alisema Houben.

Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu, Shaban Othman, akizungumza kwa niaba ya Mgeni rasmi wa hafla hiyo Mbunge wa Mbagala, Issa Mangungu alisema Serikali itaendelea kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yamekuwa yakiisaidia katika shughuli mbalimbali kama linavyofanya shirika hilo la EfG.

"Serikali imekuwa ikikaribisha wahisani na mashirika yasiyo ya kiserikali yenye nia njema ili kufanya kazi na serikali kwa lengo la kupunguza pengo lililopo serikalini na kusogeza huduma za msaada wa kisheria kwa waanchi wa Tanzania" alisema Othman.

Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita alisema utafiti uliofanywa  na shirika hilo katika masoko hayo ulionesha kuwepo kwa vitendo vya ukatili kwa asilimia 78 na pia asilimia 100 hakuna msaada wa kisheria unaotolewa kwenye masoko hayo na kuwa asilimia 85 hawa ripoti vitendo vya ukatili pindi vinapotokea sokoni kwao.


No comments:

Post a Comment