KATIKA kuadhimisha siku ya wapendano duniani
maarufu kama ‘Valentine’s Day’ Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL)
imewakutanisha wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo ikiwa ni sehemu ya kutambua
mchango wao katika utendaji kazi wa kampuni hiyo.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo Alhamisi Februari 14, 2019 Mwenyekiti wa wanawake
wa SBL, Anitha Rwehumbiza amesema lengo kubwa ni kuwainua wanawake ndani na nje
ya ofisi kupitia jukwaa maalumu lijulikanalo ‘SBL spirited women’.
Hafla hiyo imefanyika katika makao makuu ya
kampuni hiyo yaliyopo Chang’ombe jijini hapa pamoja na matawi yaliyopo mikoa ya
Mwanza na Moshi.
“Lengo
ni kuwainua wanawake katika nyanja tofauti sio tu katika kazi lakini pia nje ya
ofisi na kwa mwaka huu tumeona tujumuike
pamoja tuonyeshe upendo wetu kwa wanawake wote wa Serengeti na kuwashukuru
wanawake kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kuendeleza kiwanda chetu,” amesema
Rwehumbiza.
![]() |
Wafanyakazi wanawake maarufu kama SBL spirited women kutoka mkoani Mwanza wakiwa kwenye vazi la rangi nyekundu wakati wa siku ya wapendanao 'Valentine's Day' |
Rwehumbiza
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL amesema katika siku hiyo ya
wapendanao kampuni ya Serengeti inawakumbusha watanzania kuzingatia unywaji
kiistaraabu ili kuepusha ajali zitokanazo na ulevi hapa nchini.
“Kwa
wateja wetu tunawashukuru sana kwa kuwa pamoja na sisi kwasababu uwepo wetu
unategemea zaidi wafanyakazi na vilevile wanywaji wetu wakubwa,” amesema
Wanawake hao walionyesha umaridadi kwa kuvaa mavazi ya rangi nyekundu ambayo huvaliwa katika siku hiyo na kukabidhiwa kinywaji maalumu kijulikanacho kama ‘Baileys’
kinachotengenezwa na kampuni mama ya Diageo na kusambazwa na kampuni ya bia Serengeti.
kinachotengenezwa na kampuni mama ya Diageo na kusambazwa na kampuni ya bia Serengeti.
![]() |
Wafanyakazi wa Sereneti Breweries tawi la Moshi wakifurahi wakati wa maadhimisho ya siku ya wapendanao yaliyofanyika leo mkoani hapo |
No comments:
Post a Comment