KIKAO CHA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KILICHOFANYIKA JIJINI ARUSHA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 1 December 2018

KIKAO CHA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KILICHOFANYIKA JIJINI ARUSHA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni (katikati) akizungumza mara baada ya kuahirishwa kwa Mkutano wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha. Picha na Ikulu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiagana na  Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kikao cha cha Ndani cha 20 cha Wakuu wanchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli (kulia) akizungumza jambo katika kikao chao na Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, kushoto ni Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika kikao kilichofanyika Ikulu jijini Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wakielekea kwenye gari moja pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kikao cha cha majadiliano kilichofanyika AICC jijini Arusha.

No comments:

Post a Comment