ADC WAAHIDI KUKUZA UCHUMI WA NCHI NA PATO LA KAYA - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 20 August 2025

ADC WAAHIDI KUKUZA UCHUMI WA NCHI NA PATO LA KAYA

Na Dunstan Mhilu

CHAMA cha Alliance for Demokratic for Change (ADC) kimesema kitakapo pata ridhaa yakushika dola kutoka kwa wananchi kitatengeza mazingira rafiki ya kukuza uchumi wa nchi na pato la kaya.

 

Hayo yalielezwa leo na wagombea Ubunge wa Jimbo la Kawe na jimbo la Kinondoni mkoani Dar es Salaam, baada ya kuchukuwa fomu kwa ajili ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa Urais na Wabunge utakaofanyika Oktoba 19, 2025.

 

Wakwanza kuzungumza na blog hii baada ya uchukuaji fomu ya Ubunge ni mgombea wa ADC jimbo la Kawe , Hassan Mvungi ambapo alisema kwakifupi kawe ina kero na changamoto nyingi lakini atakapo pata ridhaa yakuongoza wananchi atatatua kero jumuishi na kuzifanya kuwa fursa.

 

“Ni ukweli usiopingika kwamba Kawe kwakipindi ambacho imetawaliwa na wabunge kutoka katika vyama mbalimbali hawajafanikiwa kutatua kero jumuishi za wanakawe ambapo kutatuliwa kwao kungeleta ahueni na afueni kwa wananchi wa kata hiyo” amesema Mvungi

 

Mvungi alisema miongoni mwa kero kubwa ya wanakawe ambayo yaweza kuwa fursa ni masoko pamoja na stendi anaamini likijengwa soko la kisasa na stendi ya Kisasa Kawe, vitatoa ajira kwa vijana, mama na makundi maalumu.

 

“Kwakuwepo mambo haya muhimu serikali itakusanya mapato na wananchi watajiingizia kipato ndiyo maana ADC inakwenda kuimarisha uchumi wa mtu mmoja moja na Taifa kwa ujumla” amesema mvungi

 

Kwakuongezea Mvungi amesema kwamba ni wakati wa wananchi wa Kawe kuchagua mtu makini, kijana mwenye nguvu na utimamu wa akili ambaye atatatua kero kadha wa kadha za jimbo hilo ikiwemo uboreshaji wa barabara, huduma za maji safi na salama na kukuza kiwango kitaaluma kwa wananfunzi wa kata hiyo na ushirikishwaji wa michezo kwa vijana.

 

Kwa upande wake mgombea wa ubunge Jimbo la Kinondoni, Pili Mohamed Majeshi amesema ameamua kugombea nafasi hiyo kupitia ADC kwakuwa ndiyo chama chenye sera madhubuti za kumkomboa mwananchi wa kawaida na hivyo kuwaomba wanakinondoni wote kumuunga mkono ili awawakilishe wanakinondoni.

 

“Siasa sikuanza leo nimeanza miaka mingi huko CCM, lakini nimeona kwanza wananichelewesha na hivyo kujiunga na chama hiki pia kwa muda mrefu na sasa ni Mwenyekiti wa Wanawake wa ADC Taifa hivyo basi hususani wakina mama wenzangu msiniangushe ni zamu ya wakina mama Kinondoni kwa pamoja tunaweza tukutane Oktoba 29 na kwenye mikutano ya Kampeni zetu” alisema Pili

 

Naye Katibu wa ADC wilaya ya Kinondoni Sandra Kudya amesema ADC Kinondoni wamejipanga madhubuti kuhakikisha jimbo hilo linakuwa mikononi mwa ADC.

 

“Siku zote sisi siyo watu wa maneno ni watu wa vitendo hivyo basi tutawaunga mkono wanakinondoni na Taifa kwa utekelezaji wa sera na ilani safi ya ADC, jambo muhimu washiriki mikutano yetu na kusoma ilani yetu ili wafanye maamuzi sahihi wakati wakupiga kura na hatimaye kuwatumikia” alisema Sandra

No comments:

Post a Comment