UVAMIZI WA WANYAMAPORI KATIKA MASHAMBA NA MAKAZI YA WANANCHI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 25 May 2022

UVAMIZI WA WANYAMAPORI KATIKA MASHAMBA NA MAKAZI YA WANANCHI

 

TAHADHARI ZA KUCHUKUA KUEPUKA MADHARA YA WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU

Wizara ya Maliasili na Utalii imepewa dhamana ya kusimamia uhifadhi wa maliasili,malikale na maendeleo ya Utalii nchini kwa kushirikiana na wadau. Sekta hii huchangia Pato laTaifa kwa asilimia 17 na zaidi ya asilimia 25 ya fedha za kigeni.


Kwa nyakati tofauti,Wizara imepokea taarifa kuhusu uvamizi wawanyamapori katika mashamba na makazi ya wananchi katika maeneo mbalimbali nchini. Katika kutatua changamoto hii, Wizara imefanya tathmini na kubaini wanyamapori hatarishi na waharibifu ni pamoja na tembo, simba, mamba na viboko ambao matukio yao yamekuwa yakijirudia hasa katika Wilaya 53 kati ya 134 nchini.


Uvamizi wawanyamapori hawa husababisha taharuki, uharibifu wa mali, majeraha na wakati mwingine vifo. Aghalabu, maisha ya wanyamapori nayo huathirika pindi wananchi wanapolipiza kisasi na kuwadhuru. Migongano hii husababishwa na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja;

  1. Mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha ukame wa muda mrefu na mafuriko;

  2. Kupungua kwa malisho kunakosababishwa na kuenea kwa mimea vamizi katika baadhi ya maeneo yaliyohifadhiwa;

  3. Uchungaji wa mifugo kwenye maeneo yaliyohifadhiwa husababisha wanyamapori kutoka kwenye maeneo yahifadhina hivyo kuongeza migongano kwenye maeneo ya wananchi;na

  4. Matumizi holela yaardhi na kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu hasa katika maeneo ya jirani na hifadhi yakiwemo shoroba na mtawanyiko wa wanyamapori.

Katika kukabiliana na migongano hiyo, Wizara inatekeleza Mkakatiwa Taifawa Kusimamia Utatuzi wa Migongano baina ya Binadamu na Wanyamapori wa mwaka 2020-2024. Sambamba na Mkakati huo Wizara inatekeleza Mwongozo wa Mbinu Rafiki za Kudhibiti Wanyamapori Wakalina Waharibifu na kuwezesha uaandaji wa mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa vijiji vilivyopembezo ni mwa maeneo yaliyohifadhiwa. Aidha,Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inafanya mapitio ya Sera ya Wanyamapori ya mwaka 2007 pamoja na Sheria na kanuni zake. Halikadhalika, Wizara inaendelea kufanya tafiti ili kubaini mbinu na mikakati bora ya kukabiliana na changamoto hii. Hatua nyingine ni pamoja na;

  1. Hatua za muda mfupi

  • Kuwajengea uwezo wananchi kwa kuwapatia mafunzo na vifaa vya kujilindaa  ambapo hadi sasa mafunzo yametolewa kwa wakufunzi 660 katika Wilaya 21 kati ya 53 zenye migongano. Wizara inaendelea kukamilisha mafunzo kwenye Wilaya zilizosalia;

  • Kuanzisha vituo 11 vya kudumu kwa Askari wanyamapori kwenye maeneo yanayoathirika zaidi ili kuimarisha usalama wawananchi na mali zao;

  • Kuimarisha kanzidata ya migongano baina ya binadamu na wanyamapori;

  •   Namba maalum za simu zimetolewa kuwezesha wananchi kutoa taarifa za matukio ya wanyamapori bila malipo ilikupata msaada wa haraka;

  • Kuhamisha wanyamapori wakali na waharibifu kutoka kwenye makazi kwenda maeneo ya hifadhi;

  • Vizimba viwili vya mfano vimejengwa Ziwa Rukwa kwa ajili ya kujikingana mamba na viboko. Wizara inafanya taratibu za kuhakikisha wadau (Halmashauri na wadau wengine) wanaviona ili waweze kwenda kujenga kwenye maeneo yao;

  • Uvunaji wa viboko hatarishi maeneo ya bwawa la Mtera na Ziwa Babati,najitihada zitaendelea kwenye maeneo mengine;na

  • Kutoa vibali vya uvunaji wa mamba katika maeneo yenye migongano.

  1. Hatua za muda mrefu

  • Kununua helikopta kwenye kila kanda ili kushughulikia matatizo kwa haraka;

  • Kuendelea kulipa kifuta jasho na machozi kwa wananchi walioathirika;

  • Kuendelea kuimarisha doria za kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu;

  • Kuanzishwa Kamati ya Kudumu ya kuandaa, kutekeleza na kusimamia mipango ya matumizi bora ya ardhi hasa katika maeneo yenye  migongano;

  • Kuwajengea uwezowananchikwakuanzishamiradiyakuongezakipato.

  • Kupendekezauanzishwajiwamtaalawanamnayakujikinganawanyamaporiwakalinawaharibifukatikashulezangazizote;na

Pamoja na jitihada zinazoendelea kutolewa,Wizara inapenda kuwakumbusha wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya hifadhi za wanyamapori kuzingatia yafuatayo:

  1. Maelekezo yanayaotolewa nawataalamu wa Uhifadhi ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na wanyamapori wakali nawaharibifu;

  2. Wananchi kujiepusha kuwasogelea wanyamapori;

  3. Kuchukua tahadhari kufanya shughuli za kibinadamu katika maeneo au pembezoni mwa hifadhi; maeneo yenye mamba na viboko;mapito na mtawanyiko wa wanyamapori.

  4. Kujiepusha na tabia ya kupambana nawanyamapori wanapoingia kwenye maeneo yao;

  5. Kutoshiriki katika zoezi la kufukuza wanyamapori wakali na waharibifu kwa wazee,watoto,wajawazito,wenye changamoto mbalimbali za ulemavu,na waliotumia kilevi;

  6. Kuepuka matembezi yasiyo ya lazima nyakati za usiku kwa wananchi waishio pembezoni mwa maeneo yaliyohifadhiwa na ikibidi watembee zaidi ya mtu mmoja;

  7. Kuepuka uvuvi hatarishi hususani kuvua nyakati za usiku na matumizi ya vifaa duni;na

  8. Kutoa taarifa za matukio ya uvamizi wawanyamapori wakali na waharibifu haraka kupitia namba za kupiga simu bure zilizotangazwa na Wizara.

Na.

Kituo

Namba za kupiga simu bure

1

Wizara ya Maliasili na Utalii - Dodoma

0800 110 076

2

Hifadhi ya Ngorongoro

0800 110 087

3

TAWA Makao Makuu (Morogoro)

0800 110 093

4

TAWA – Kanda ya Kati (Manyoni)

0800 110 089

5

TAWA – Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Iringa)

0800 110 090

6

TAWA - Kanda ya Kusini Mashariki (Masasi)

0800 110 067

7

TAWA – Dar es Salaam na Pwani

0800 110 098

8

TAWA – Kanda ya Kusini Mashariki (Tunduru)

0800 110 054

9

TAWA - Kanda ya Magharibi (Tabora)

0800 110 048

10

TAWA - Kanda ya Kaskazini (Arusha)

0800 110 027

11

TANAPA –Kanda ya Mashariki (Mikumi)

0800 110 099

12

TANAPA - Kanda Kusini (Mbalali)

0800 110 068

13

TANAPA – Kanda ya Magharibi (Bunda)

0800 110 059

14

TANAPA – Kanda ya Kaskazini (Mkomazi)

0800 110 046


HITIMISHO

Serikali itaendelea kutoa kifuta jasho na machozi kwa mujibu wa taratibu za kisheria kwa wananchi wote walioathirika na watakaoathirika. Aidha, Serikali itaendelea na jitihada za kudhibiti na kukomesha matukio haya. Wizara inatoa pole kwa wananchi wote walioathirika kwa namna mbalimbali kutokana na mgongano baina ya binadamu na wanyamapori. Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha kuwa wananchi na mali zao wanakuwa salama kila mahali.


Imetolewa na:

Mhe.Balozi Dkt.Pindi Chana (MB)

Waziri – Wizara ya Maliasili na Utalii



No comments:

Post a Comment