WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI KUMBUKUMBU ZA MAUAJI YA KIMBARI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 8 April 2019

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI KUMBUKUMBU ZA MAUAJI YA KIMBARI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa pili kulia) akiwa na viongozi wa mataifa mbalimbali wakitoa heshima katika eneo la kumbumbu ya mauji ya kimbari, Waziri Mkuu yupo Kigali Rwanda akimwakilisha, Rais Dk. John Magufuli katika kumbumbu ya miaka 25 ya mauji ya kimbari yaliyotokea 1994.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akibadilishana Mawazo na Rais Mstaafu wa Naigeria Olusegun walipo kutana Aprili 7, 2019 katika Mji wa Kigali wakati anamwakilisha, Rais Dk. John Magufuli katika kumbumbu ya miaka 25 ya mauji ya kimbari yaliyotokea 1994.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa walipo kutana Jijini Kigali kwenye kumbumbu ya miaka 25 ya mauji ya kimbari yaliyotokea 1994.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati) akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Balozi Richard Sezibera (kulia) aliyempokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali. Waziri Majaliwa yupo nchini humo kumwakilisha Rais Dk. Magufuli katika kumbumbu ya miaka 25 ya mauji ya kimbari yaliyotokea 1994, Kushoto ni Balozi wa Tanzania Nchini Rwanda, Balozi Ernest Mangu.  (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kudumisha amani, umoja na mshikamano ambavyo ni tunu walizoachiwa na waasisi wa Taifa. Ameyasema hayo Aprili 7, 2019 katika kumbukumbu ya miaka 25 ya mauaji ya Kimbari iliyofanyika katika jiji la Kigali nchini Rwanda.

Waziri Mkuu ambaye amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika kumbukumbu hizo, amewasisitiza Watanzania kudumisha amani na utulivu.

Awali,Waziri Mkuu alijumuika na viongozi kutoka nchi mbalimbali kutoa heshima kwenye eneo la kumbukumbu ya mauaji hayo la Gisozi lililopo jijini Kigali.

Baada ya kutoa heshima kwenye eneo la kumbukumbu za mauaji hayo, Rais wa Rwanda, Paul Kagame alitoa maelezo ya kina kuhusu mauaji hayo yaliyotokea Rwanda 1994.

Viongozi wengine waliohudhuria kumbukumbu hizo ni pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa Nigeria, Ulusegun Obasanjo.

No comments:

Post a Comment