 |
| Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Daniel Chongolo (kulia) akimkabidhi cheti cha Balozi mzuri wa Benki yaNMB mfanyabiashara, Patricia Pancras Rweyendela kilichotolewa na benki hiyo kwa baadhi ya wafanyabiashara wa kupigiwa mfano. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard pamoja na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd wakishuhudia. |
 |
| Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Daniel Chongolo (kulia) akimkabidhi cheti cha Balozi mzuri wa Benki yaNMB mfanyabiashara, Beatrice Jackson (Amazing Interiors B+RC Ltd) kilichotolewa na benki hiyo kwa baadhi ya wafanyabiashara wa kupigiwa mfano. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard pamoja na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd wakishuhudia. |
 |
| Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Daniel Chongolo (kulia) akimkabidhi cheti cha Balozi mzuri wa Benki yaNMB mfanyabiashara, Arnold Mwasumbi kilichotolewa na benki hiyo kwa baadhi ya wafanyabiashara wa kupigiwa mfano. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard pamoja na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd wakishuhudia. |
 |
| Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard (katikati) akizungumza na wafanyabiashara katika kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilaya za Kinondoni na Ubungo jijini Dar es Salaam. Kulia ni mgeni rasmi katika Kongamano hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Daniel Chongolo pamoja na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd (kushoto). Kongamano hilo liliandaliwa na Benki ya NMB kutoa elimu kwa wafanyabiashara. |
 |
| Sehemu ya wafanyabiashara katika kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilaya za Kinondoni na Ubungo jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye Kongamano hilo liliandaliwa na Benki ya NMB kutoa elimu kwa wafanyabiashara. |
BENKI ya NMB imepanga kuhakikisha inafanikisha kuwapeleka baadhi ya wafanyabiasha nchini nje ya nchi kushiriki katika maonesho ya biashara kimataifa ili kujifunza zaidi namna wengine walivyofanikiwa.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya NMB, Donatus Richard alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara katika kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilaya za Kinondoni na Ubungo jijini Dar es Salaam waliokutanishwa na NMB kupata mafunzo kuboresha biashara zao.
"...Miongoni mwa mambo ambayo tumejipanga kuyafanya mwaka huu ni kuhakikisha tunawapeleka baadhi ya wafanyabiashara wateja wetu kwenye maonesho ya biashara kimataifa nje ya nchi ili wajifunze zaidi na kupata uzoefu," alisema Bw. Richard akizungumza katika kongamano hilo.
Alisema masuala mengine ni pamoja na kuongeza mafunzo kwa kundi maalum la wafanyabiashara akinamama ili kuhakikisha wanainuliwa zaidi katika biashara zao.
Alisema kiujumla mwaka huu mafunzo kwa wafanyabiashara wateja wao yatajikita katika elimu ya masoko ili waweze kukabiliana na changamoto za masoko ambazo zimekuwa kikwazo kwa walio wengi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Daniel Chongolo ambaye alikuwa mgeni rasmi, akifungua kongamano hilo alisema Serikali inafarijika kuona taasisi za kibenki kama Benki ya NMB ikitoa mafunzo kwa wafanyabiashara kwani kukua kwa kundi hilo kiuchumi ni kukua kwa pato la Serikali pia kupitia kodi.
Aliipongeza Benki ya NMB kuendelea kuwakutanisha wafanyabiashara kupitia Klabu za Biashara za NMB na kutoa mafunzo kwani mafunzo hayo ni muhimu sana kwani mbali na kukuza biashara zao wanajifunza namna ya kuwa walipaji wazuri wa kodi za Serikali na kukuza pato la taifa tena. Hadi sasa Benki ya NMB ina Klabu 36 za wafanyabiashara nchi nzima zinazonufaika na fursa anuai za kibiashara.
No comments:
Post a Comment