DKT. MWIGULU AKUTANA NA MAWAZIRI WA MAJI NA FEDHA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 3 January 2026

DKT. MWIGULU AKUTANA NA MAWAZIRI WA MAJI NA FEDHA


WAZIRI Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 03, 2026 amefanya mazungumzo na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso  na Waziri wa Fedha, Balozi,  Khamis Omar katika kikao cha kazi kilichofanyika ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Januari 3, 2026. 

Kikao hicho pia kiliwahusisha viongozi na watendaji kutoka TAMISEMI, Wizara ya Fedha na Wizara ya Maji.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu, Dkt. Nchemba Januari 03, 2026 pia amefanya mazungumzo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe,  ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Januari 3, 2026. 

Viongozi wengine walioshiriki kikao kazi hicho ni Katibu Mkuu  (OWM-TAMISEMI), Adolf Ndunguru  (OWM-TAMISEMI), Naibu Katibu  Mkuu  (OWM-TAMISEMI), Sospeter Mtwale pamoja na na Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa, Beatrice Kimoleta.



No comments:

Post a Comment