Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi
Deusdedit C.V. Kakoko akitoa taarifa ya Mpango wa Kitaasisi na Utendaji
wa Bandari ya Tanga kwa Mwaka wa Fedha 2018/19 na Nusu Mwaka ya Kwanza
ya Mwaka wa Fedha 2019/2020 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji
wa Mitaji ya Umma (PIC) ilipotembelea Bandari ya Tanga hivi karibuni.
Sehemu ya wajumbe wa kamati hiyo wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deusdedit C.V. Kakoko akipata maelezo
Sehemu ya wajumbe wa kamati hiyo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi
Deusdedit C.V. Kakoko katikati akiwaongoza wajumbe wa kamati hiyo
kutembelea maeneo mbalimbali ya Bandari hiyo
KAMATI ya Bunge ya Kudumu ya Uwekezaji wa Mitaji ya Serikali Umma (PIC)
imeipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa
kutekeleza kwa ufanisi maboresho na miradi mbalimbali katika Bandari ya
Tanga.
Maboresho
ya miradi hiyo hususani mradi wa kuchimba na kuongeza kina cha gati ya
Bandari hiyo lengo likiwa ni kuongeza tija, ufanisi pamoja na ushindani
na nchi jirani zenye Bandari.
Lengo
la ziara ya Kamati ya PIC ilikuwa ni kuangalia kama uwekezaji wa
mitaji ya Serikali unaleta manufaa yaliyokusudiwa na kutoa ushauri wa
kimkakati wa namna ya kusaidia katika kuongeza thamani ya mitaji husika
inayotewa na Serikali.
Pamoja
na kutembelea meli maalum ya kuchimbia (Dredging Vessel) na kujionea
wenyewe shughuli za uchimbaji na kuongeza kina zinavyoendelea
walitembelea pia miradi ifuatayo:-
• Mradi wa Ukarabati wa Miundombinu na Majengo Bandarini
• Mradi wa maboresho wa gati la mafuta Ras Kazone.
No comments:
Post a Comment