WAFANYAKAZI BENKI YA NMB WASAIDIA VITUO VIWILI VYA WATOTO YATIMA DAR - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 9 February 2019

WAFANYAKAZI BENKI YA NMB WASAIDIA VITUO VIWILI VYA WATOTO YATIMA DAR

Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto) akimkabidhi Sista Deepty Grace (kulia) kutoka kituo cha Watoto Yatima cha Mama Teresa cha Kigogo Mburahati kilichopo jijini Dar es Salaam sehemu ya msaada uliotolewa na wafanyakazi wa Benki ya NMB.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiingiza ndani ya kituo sehemu ya misaada waliokabidhi leo katika kituo cha Watoto Yatima cha Mama Teresa cha Kigogo Mburahati kilichopo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiwa katika picha ya pamoja kwenye kituo cha Watoto Yatima cha Mama Teresa cha Kigogo Mburahati kilichopo jijini Dar es Salaam mara baada ya kukabidhi misaada yao.
Na Mwandishi Wetu

WAFANYAKAZI wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam leo wametembelea vituo viwili vya watoto vya watoto yatima na kutoa misaada mbalimbali. Vituo vilivyotembelewa ni pamoja na Kituo cha Mama Teresa cha Kigogo Mburahati na Kituo cha Watoto yatima cha Kurasini vyote vya jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kituo cha yatima cha Mama Teresa, Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi alisema msaada huo umetolewa na wafanyakazi wa benki hiyo, ikiwa ni utaratibu wao wa kawaida kusaidia jamii.

Alisema vitu vilivyotolewa ni pamoja na nguo na viatu vya watoto kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea. Vingine ni pamoja na vifaa vya kuchezea watoto, mafuta ya kula na sabuni za kufulia. "..Huu ni utaratibu wa kawaida kabisa kujitolea kwa wafanyakazi wetu, leo tumekuja na kujumuika na watoto wa vituo hivi viwili na kuleta hiki tulichojaliwa ambacho kimetolewa na wafanyakazi wenzetu," alisema Bw. Mponzi.

Akizungumza kushukuru msaada huo, mama mlezi wa kituo yatima cha Kurasini mara baada ya kupokea msaada huo, alisema wamefarijika kupokea msaada kwa wahitaji na kuwaomba wafanyakazi wa NMB kuendelea kuwa na moyo wa kuguswa na kusaidia wahitaji.

Aidha ameomba taasisi na makampuni mengine kufuata nyayo za Benki ya NMB kusaidia jamii hasa wahitaji kama vituo vya yatima na wasiojiweza.

No comments:

Post a Comment