
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa Bungeni kabla ya kuhutubia.
Na Dotto Mwaibale, Dodoma
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi kuchuja makosa ya vijana walioshtakiwa kwa makosa ya uhaini kufuatia maandamano ya Oktoba 29, 2025 na kwa wale waliofanya makosa kwa kufuata mkumbo waachiwe
Dkt. Samia ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ametoa msamaha huo leo Novemba 14, 2025 alipokuwa akihutubia na kufungua rasmi shughuli za Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais Dkt Samia ametoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na Usalama hususani Ofisi ya DPP kuchuja makosa ya Vijana walioshtakiwa kwa makosa ya uhaini kufuatia maandamano ya Oktoba 29,2025 kwa wale waliofanya kwa kufuata mkumbo waachiwe huru.
“Natambua kuna vijana wengi wamekamatwa kwa kushtakiwa kwa makosa ya uhaini hawakujua wanachokifanya na wengine wamefuata mkumbo, nikiwa kama Mama navielekeza vyombo vya kisheria kuangalia makosa yaliyofanywa na Vijana wetu, kwa wale ambao walifanya mambo kwa kufuata mkumbo na hawakudhamiria kufanya uhalifu wawafutie makosa yao,” alisema Dk.Samia
“Ukiangalia 'clip' zile za maandamano unaona kabisa kuna Vijana waliingia kwa kufata mkumbo, wanaimba kwa ushabiki, naelekeza Ofisi ya DPP kuchuja viwango vya makosa na kwa waliofuata mkumbo wawaachie waende kwa Wazazi wao,”
Aidha Dkt. Samia ametumia nafasi hiyo kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki walioathirika na maandamano hayo yaliyosababisha vifo na uharibifu wa mali.
"Mimi binafsi, waheshimiwa wabunge nimehuzunishwa sana na tukio lile, natoa pole kwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao. Na tunaomba Mwenyezi Mungu awapumzishe kwa amani na kwa majeruhi tunawaombea wapone,” alisema Dkt. Samia.
Katika hutuba hiyo Dkt. Samia alizungumzia mipango mbalimbali ya maendeleo ya Serikali itakayotekelezwa katika sekta za elimu, madini, ukuzaji wa uchumi, kuwajengea uwezo vijana na kuanzisha wizara yao na mambo mengine mengi.
Taswira ya bunge kabla ya kufunguliwa kwa shughuli zake kwa hutuba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba akiwa bungeni.
Wabunge wakiwa bungeni.
Wabunge wakiwa wamesimama kwa dakika moja kufuatia vifo vya wananchi waliofariki katika maandamano ya Oktoba 29, 2025 wakati wa uchaguzi mkuu.
Wabunge wakiwa bungeni.
Wageni mbalimbali wakiwa bungeni kushuhudia ufunguzi rasmi wa shughuli za bunge la 13.
Wageni mbalimbali wakiwa bungeni kushuhudia ufunguzi rasmi wa shughuli za bunge la 13.




.jpeg)







No comments:
Post a Comment