MGOMBEA MWENZA URAIS NAFASI YA CCM, BALOZI DKT. NCHIMBI AHUTUBIA WAKAZI WA MJI MDOGO WA ISAKA WILAYANI KAHAMA, JIMBO LA MSALALA, MKOANI SHINYANGA. - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 4 September 2025

MGOMBEA MWENZA URAIS NAFASI YA CCM, BALOZI DKT. NCHIMBI AHUTUBIA WAKAZI WA MJI MDOGO WA ISAKA WILAYANI KAHAMA, JIMBO LA MSALALA, MKOANI SHINYANGA.

 










MGOMBEA Mwenza Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi  akiwahutubia Wakazi wa mji mdogo wa Isaka wilayani Kahama, jimbo la Msalala,kwenye mkutano mdogo wa hadhara leo Alhamis Septemba 4, 2025, mkoani Shinyanga.

Pamoja na mambo mengine Dkt Nchimbi pia aliwanadi wagombea Ubunge,akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Msalala Mabula Johnson Magangila pamoja na Madiwani. 

Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya Kampeni Mkoani Shinyanga ya kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030, ambayo inalenga kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29, 2025.

No comments:

Post a Comment