Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwa la msingi kuashiria ukarabati wa majengo ya Chuo cha Ualimu Kitangali kilichopo Newala Vijijini akiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichaki, Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamela O'Donnell na viongozi wengine Jumatano Aprili 3, 2019. Mradi wa ukarabati wa chuo hicho ni moja ya miradi inayohusisha ukarabati wa vyuo vya ualimu nchini vikiwemo vya Ndala, Shinyanga na Mpuguso kwa gharama ya shilingi bilioni 36.475 ikiwa ni ufadhili wa serikali ya Canada iliyotoa shilingi bilioni 28.275 wakati serikli ya Tanzania imetoa shilingi bilioni 8.200. |
No comments:
Post a Comment